Duration 11:13

Ufugaji wa kuku wenye tija.Jifunze njia 10 za kupunguza gharama ya chakula cha kuku

7 652 watched
0
39
Published 2 Nov 2021

Jifunze Jinsi ya Kutengeneza Chakula Cha Kuku cha gharama nafuu Vyakula vya kuku vinaweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe. Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa. Chakula hicho lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile protini, wanga, madini na vitamini. Hakikisha chakula unachotengeneza kina mchanganyiko wa vyakula vifuatavyo: · Vyakula vya kujenga mwili kama vile jamii ya kunde, samaki, dagaa, mashudu ya ufuta, pamba na alizeti. · Vyakula vya kulinda na kukinga mwili usipate maradhi kama vile mafuta ya samaki na majani mabichi kama kabichi, michicha, majani ya mpapai na nyasi mbichi. · Vyakula vinavyojenga mifupa kama vile aina ya madini, chokaa, mifupa iliyosagwa na chumvi. Ukosefu wa vitamini na madini kama Kalsiamu na Fosforasi husababisha matege, kukunjamana kwa vidole, kufyatuka kwa misuli ya goti na kupofuka macho. Maji ni muhimu sana kwani husaidia kulainisha na kurahisisha usagaji wa chakula, na kupunguzajoto. Wakati wajoto kali kuku wapewe maji mengi. Kabla ya Kutengeneza Chakula Lazima Mtengenezaji Ajue haya Yafuatayo:- · Jinsi ya kupata vyakula vya aina mbali mbali. · Kiasi cha viinilishe vinavyohitajika kwa kuzingatia umri na aina tofauti ya kuku; kwa mfano vifaranga wanahitaji protini asilimia 18 hadi 22, kuku wanaokua asilimia 17 hadi 19 na kuku wa mayai asimilia 15 hadi 17. Vile vile madini aina ya Kalsiamu kiasi cha asilimia tatu hadi nne kinahitajika kwa kuku wa mayai na asilimia moja kwa kuku wa nyama na vifaranga. · Viwango vya uchanganyaji wa aina za vyakula mbali mbali: Ili mtengenezaji aweze kutengeneza chakula bora ni muhimu afuate kiwango cha uchanganyaji kilichopendekezwa Kiasi cha aina moja ya chakula kinapozidi kinaweza kuleta madhara. #mkulimasmart #shambadarasa JIFUNZE KANUNI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA ... UFUGAJI WA KUKU:Jinsi ya kuaandaa chakula cha kuku na ... Uchanganyaji wa Chakula Cha Kuku wa Kienyeji - Kienyeji ... Mkulima atengeneza chakula cha kuku kutoka kwa mayai ya Nzi JINSI YA KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU NAMNA YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA KUKU-1 JINSI YA KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU WA ... Mchanganyiko wa Chakula cha kuku | njia rahisi ya kutengeneza chakula cha kuku wako (layers na ... Jinsi ya Kutengeneza Chakula Cha Kuku. kutengeneza chakula cha kuku pdf ratiba ya chakula cha kuku wa kienyeji chakula cha kuku wa mayai chakula cha kuku sasso aina ya chakula cha kuku chakula cha kuku kulingana na umri chakula cha vifaranga wa kienyeji bei ya chakula cha kuku

Category

Show more

Comments - 17